
Kai Havertz wa Chelsea (kulia) akimtoka mchezaji wa Everton
Tuchel ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Everton kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza uliopigwa usiku wa kuamkia leo Machi 9, 2021.
"Nimefurahishwa sana na Kai. Ilikuwa ni imani tuliyompa na alitumia uaminifu huo, ana uwezo wote wa kuwa mtu mashuhuri katika eneo la ushambuliaji," amesema Tuchel.
Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel
Ameendelea kumimina sifa kwa Kai ambaye ni mjerumani mwenzake kwa kusema, "Muda wote alikuwa anaonekana kwenye safu ya ushambuliaji akisaidia kuongeza kasi ya mashambulizi jambo lililotusaidia''.
Tuchel sasa ameiongoza Chelsea katika michezo 11 bila kupoteza, tangu alipochukua nafasi ya Frank Lampard ambaye alitimuliwa mwezi Januari mwaka huu.