"Tumepewa $3500 kati ya $1 milioni" - msemaji ZFF

Jumatatu , 18th Mei , 2020

Msemaji wa Shirikisho la Soka la Zanzibar ZFF, Adam Natepe amesema kuwa wamefanya juhudi kubwa kuongea na Shirikisho la Soka Tanzania TFF juu ya haki zao za fedha za FIFA lakini wenzao wanaonesha kiburi.

TFF na ZFF

Akiongea na EATV & EA Radio Digital, Natepe amesema kuwa haki ya fedha zao iko katika katiba ya mashirikisho yote mawili hivyo, TFF warejee katika katiba na kusoma makubaliano yao ili wapewe stahiki kwa mujibu wa kanuni.

"Yapo mambo baadhi serikali ya Tanzania na serikali ya Zanzibar yanakaa pamoja kuyashughulikia na yanakwenda vizuri, sasa kwanini sisi huku tunakuwa tunakwama. Yeye ni kama msimamizi wa mali za familia, siyo yake ila ni ya familia", amesema Natepe.

"Katika mipango ya FIFA Forward 1 na FIFA Forward 2, sisi tuliyopewa haizidi Dola za Kimarekani 3500 kati ya Dola milioni moja zinazokuja lakini ukiangalia malengo ya ile FIFA Forward 1 yote sisi tunayo", ameongeza.

Mtazame zaidi katika video hapa chini.