picha ya pamoja ya kocha Zinedine Zidane na Gareth Bale
Real Madrid watatwaa ubingwa wa LaLiga kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu na wa 34 katika historia ya klabu kama wakiifunga Villarreal leo usiku.
kuelekea mchezo huu zidane aliulizwa kuhusu Bale ambaye imekuwa ikiripotiwa kuwa hawana mahusiano mazuri, alisisitiza kwa sasa wanafikiria zaidi kuhusu ubingwa wa LaLiga.
Gareth Bale raia wa Wales ambaye anatimiza miaka 31 leo hajacheza hata dakika moja kwenye michezo 5 iliyopita na kwenye moja ya mchezo alionekana akiwa amelala jukwaani kwa kujifunika barakoa machoni mchezo ukiwa unaendelea licha ya kuwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba. Msimu huu winga huyo amecheza michezo 20 katika mashindano yote na amefunga mabao 3 tu.
Imekuwa ikiripotiwa kuwa zidane hamtaki Bale kwenye kikosi chake, lakini Wakala wa mchezaji huyo Jonathan Barnett amekuwa akisisitiza mchezaji wake haondoki Real Madrid.
Bale alijiunga na Real Madrid mwaka 2013 akitokea Tottenham Hotspur mkataba wake na Real Madrid unamaliza June 30 2022.


