
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga klabu ya Mansfield Town Abdillah Yusuph
Morocco amesema, katika mchezo wa marudiano dhidi ya Chad utakaopigwa siku ya Jumatatu ya Machi 28 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watamuangalia namna atakavyoitumia nafasi yake kwani wanaamini anauwezo wa kuisaidia Taifa Stars kuweza kufanya vizuri.
Hemed Morocco amesema, katika mchezo wa awali uliopigwa Jumatano ya machi 23 nchini Chad walienda wakijua wanaenda kucheza ugenini hivyo walijipanga kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ili kujiweka salama zaidi katika mchezo wa marudiano.
Morocco amesema, walipata athari kutokana na hali ya hewa ya nchini Chad kuwa ya joto sana lakini walijitahidi kucheza katika kipindi cha kwanza na kuweza kupata goli moja lakini katika kipindi cha pili cha mchezo hali ya hewa ilizidi kuwaathiri lakini waliweza kujitahidi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo wa kundi G mechi ya kufuzu michuano ya Afrika 2017 nchini Gabon.