Ijumaa , 27th Aug , 2021

Muendesha magari wa mashindano ya Langalanga kutoka kampuni ya Mercedes, Valterri Bottas amemshinda mpinzani wake Max Vestarppen kutoka  Red Bull katika mazoezi ya kwanza ya mashindano ya Belgium Grand Prix huku  Lewis Hamilton kutoka kampuni ya Mercedes akimaliza nafasi ya 18.

Valterri Bottas (Kushoto) akiwa na Lewis Hamilton (Kulia).

Bottas aliendesha kwa haraka  akitumia  sekunde 0.164 kuliko Verstappen, ambaye alishika nafasi ya pili huku, nafasi ya tatu ikienda kwa Pierre Gasly kutoka kampuni ya Alphatauri Honda.

Vilevile Bottas amemshinda bingwa mara saba wa mashindano hayo Lewis Hamilton, alilazimika kutokumaliza raundi ya mwisho ya mashindano hayo baada ya kunusurika kwenye ajali baada ya kufuatia kukongana na Nicholas Lafiti kutoka kampuni ya Williams Mercedez ambaye alimaliza nafasi ya 16. 

Kilele cha mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika siku ya jumapili Agosti 29, 2021 huku timu 12 zikitajaria kufuzu kwenye hatua ya mwisho baada ya hatua mbili za mchujo kuisha.