
Bao la dakika za majeruhi la Adrian Lopez, liliipa Villarreal ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Europa League.
Liverpool walikosa bao kupitia kiungo Joe Allen shuti la mita 12 lililookolewa na mlinda mlango wa Villarreal Sergio Asenjo, huku pia mlinda mlango huyo akizuia shuti la mshambuliaji Roberto Firmino kunako kipindi cha pili.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa alhamisi ijayo kwenye uwanja wa Anfield.