Jumatano , 20th Jan , 2021

Manchester United na Manchester City, zinashuka dimbani leo kusaka alama tatu muhimu na wapinzani tofauti, matokeo yanayoweza kubadili msimamo wa ligi hasa kwenye nafasi ya kwanza, ambayo inashikiliwa na Leicester City.

Makocha toka jiji la Manchester Ole Gunnar Solskjaer na Pep Guardiola wanaowania uongozi wa ligi EPL

Manchester City yenye alama 35 itakuwa nyumbani uwanja wa Etihad kukipiga na Aston Villa yenye alama 26, ikionekana kuimarika sana msimu huu, ukifananisha na msimu uliomalizika wa 2019/2020 ambayo al manusura iporomoke daraja.

Manchester United wenyewe wana alama 37 ipo kwenye nafasi ya pili nyuma ya vinara Leicester City, yenye alama 38 ngoza ligi hiyo, itakuwa kibaruani ugenini katika uwanja wa Craven Cottege kupambana na Fulham.

Matokeo ya ushindi wa timu hizi kutoka jiji la Manchester, moja kwa moja zitawafanya kuongoza ligi kwa muda, endapo United atashinda basi atafikisha alama 40 na kuwa vinara wa ligi, endapo atatoa sare au kupoteza huku City akishinda ataongoza ligi kwa alama 38 sawa na Leicester City ila yeye ana wastani mzuri wa magoli.