Jumatatu , 21st Jun , 2021

Ligi kuu soka Tanzania bara inaendelea tena leo kwa michezo miwili raundi ya 32, KMC watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Saa 8:00 Mchana na Namungo wanawaarika Azam FC mchezo utakao chezwa Saa 10:00 jioni.

Matukio mchezo wa mwisho Azam walipokutana na Namungo Mkoani Lindi

KMC watakuwa wanautafu ushindi wa kwanza baada kushindwa kupata ushindi kwenye michezo minne iliyopita baada ya kufungwa michezo miwili liyopita na kutoka sare michezo miwili, kikosi hicho kutoka Manispaa ya kinondoni kipo nafasi ya saba wakiwa na alama 41.

Wapinzani wao Mtibwa Sugar wana alama 37 wapo nafasi ya 12 na wapo kwenye kiwango bora kwani wameshinda michezo mitatu mfululizo iliyopita. Mchezo wa mkondo wa kwanza ulimalizika kwa Mtibwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo mwingine unachezwa uwanja wa Majaliwa ambapo Namungo watakuwa wakicheza dhidi ya Azam. Mchezo wa kwanza timu hizi zilitoka sare ya mabao 2-2. Azam wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na alama 63 na hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye michezo 10 ya mwisho, wameshinda michezo nane na wamesare michezo miwili.

Wenyeji Namungo wapo nafasi ya sita wakiwa na alama 42, na hawajashinda mchezo hata mmoja katika michezo mitatu ya mwisho wamefungwa mchezo mmoja na wametoka sare michezo miwili.