Wachezaji Man United walifurahia kupangwa na Barca

Jumanne , 9th Apr , 2019

Beki wa Manchester United, Chris Smalling amesema kuwa yeye na wachezaji wenzake walifurahia kupangwa na Barcelona katika mchezo wa Robo Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.

Man United na Barcelona

Manchester United waliwashangaza wadau wa soka duniani waliokuwa wakiamini hawana uwezo wa kusonga mbele katika hatua ya mtoano, baada ya kupindua matokeo dhidi ya PSG katika mchezo wa marudiano Jijini Paris.

Vijana hao wa Ole Gunnar Solskjaer waliweka historia kwenye historia ya Klabu Bingwa Ulaya kuwa klabu ya kwanza kukubali kufungwa mabao 2-0 nyumbani kisha kupindua ugenini na kufuzu hatu ainayofuata.

Kufuatia muendelezo huo, Smalling amesema kuwa yeye na wachezaji wenzake walikuwa wakihitaji aina ya timu hiyo waliyopangiwa.

"Katika droo zetu zote msimu huu, iwe ni FA au Klabu Bingwa, hatujawa na droo rahisi lakini tumefanikiwa kuzivuka timu zote tulizopangwa nazo", amesema Smalling.

"Baada ya mchezo na PSG, tulijua kuwa tunaweza kwenda kukutana na timu kubwa na tukapata ushindi. Macho yetu yote sasa ni juu ya mchezo unaokuja mbele yetu, tutakabiliana nao".

"Tulikuwa tukipasha katika baiskeli wakati wa gym . Kwa kawaida tunafanya mazoezi dakika 10 kwenye baiskeli na baadaye katika gym, tuliiona droo katika TV na tulifurahi ", ameongeza.

Manchester United na Barcelona zitakutana kesho Jumatano katika dimba la Old Trafford.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.