Wachezaji wa Simba walioondolewa kwenye kikosi

Jumanne , 11th Feb , 2020

Kikosi cha Simba kinatarajia kushuka dimbani hii leo, Februari 11 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Wachezaji wa Simba wakiwa mazoezini

Kuelekea mchezo huo, Simba imetoa taarifa ya kikosi kilichokuwa fiti hii leo, ambapo jumla ya wachezaji wawili wameachwa Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wachezaji walioachwa ni Mzamiru Yassin na Miraji Athuman ambao wanaendelea na matibabu  baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga, Januari 04.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 50 baada ya kushuka dimbani michezo 20 huku Mtibwa Sugar ikiwa katika nafasi 13 na pointi 23, baada ya kushuka dimbani michezo 20.