Jumapili , 25th Nov , 2018

Shirikisho la Soka Tanzania TFF kupitia kwa Kamati ya Uchaguzi imepitisha majina ya wagombea wa nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya klabu ya Yanga.

Makao Makuu ya Yanga

Majina hayo yaliyopitishwa ni katika nafasi za Mwenyekiti wa klabu, Makamu Mwenyekiti na zile za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Kwa upande wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu, waliopitishwa ni Dkt. Jonas Tiboroha, Mbaraka Igangula na Erick Ninga. Kwa wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu, waliopitishwa ni pamoja na, Yono Kevela, Titus Osoro na Salum Chota.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, waliopitishwa ni 16 ambao ni Hamad Ally Islam, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvestre Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige.

Walioenguliwa ni Pindu Luhoyo, Mussa Katabaro ambaye hakurudisha fomu, Geoffrey Boniface Mwita na Justin Peter Bisangwa ambao wamekosa sifa za uzofu. Baada ya hapo, zoezi litakalofuata ni Kamati ya Uchaguzi kupokea mapingamizi juu ya wagombea hadi Novemba 25 na kuyapitia na kuwafanyia usaili wagombea hadi Novemba 28.

Desemba 11 hadi 14 Kamati ya Maadili itatangaza uamuzi wa masuala ya Kimaadili iliyoyajadili, kabla ya kutoa fursa ya wagombea walioathirika na zoezi hilo kukata Rufaa na Januari 4 hadi 6 orodha kamili ya mwisho ya wagombea itatolewa baada ya michakato yote tayari kwa kampeni kati ya Januari 8 na 12.

Zoezi linalosubiriwa hivi sasa ni la mapingamizi pekee kabla ya kuelekea kwenye kampeni na baadaye uchaguzi ambao utafanyika Januari 13, 2019.