Jumanne , 6th Dec , 2016

Aliyekuwa kocha Mkuu wa timu ya Wajelajela Tanzania Prisons Abdul Mingange amesema, kwa sasa yupo tayari kufanya kazi na timu yoyote itakayomuhitaji mara baada ya kuachwa na Wajelajela hao wa jijini Mbeya.

Abdul Mingange

Kocha Mingange amesema, kwa upande wake anajua alikuwa anafanya vizuri kazi yake na alikuwa na mategemeo na timu hiyo kusonga mbele zaidi ya hapo ilipo lakini kutokana na hali iliyotokea ameamua kukubaliana nayo na anaendelea kusubiria malipo yake ya miezi miwili.

"Nimeshapewa uhuru na uongozi wa Prisons japo sijaambiwa sababu kwani bado nilikuwa kuendelea kukipeleka kikosi mbele zaidi ya kilipo sasa lakini kwa sasa nipo tayari kufanya kazi ya kuendelea kufundisha soka ambalo ndiyo kazi yangu na lengo langu hasa ni kuendelea kukuza soka la vijana," amesema Mingange.