Alhamisi , 13th Feb , 2020

Huenda ule utawala wa Singida United na baadhi ya vigogo wengine katika Ligi Kuu Tanzania Bara ukaelekea kukatika, baada ya kudumu kwa takribani misimu mitatu na zaidi.

Uwanja wa Taifa

Singida United bado haioneshi kujinasua kutoka mkiani, kwani mpakam sasa ina pointi 11 na imeshinda mechi mbili pekee kati ya 21 ilizocheza, ikipoteza mechi 14 na sare tano.

Msimu huu jumla ya timu nne zitashuka daraja moja kwa moja na timu mbili zikitakiwa kucheza hatua ya mtoano ili kubakia katika ligi endapo watashinda. Singida United ipo katika nafasi ya 20, Mbeya City  ipo katika nafasi ya 19, Mwadui FC nafasi ya 18 na nafasi ya 17 ikishikiliwa na Mbao FC.

Kuanzia timu iliyo nafasi ya 11 hadi ya 20 zipo katika hatari ya kushuka daraja kwani zimepishana kwa tofauti ya pointi 15, huku msimu huu ukishuhudiwa vigogo wengi wakiwa katika hatari hiyo.

Singida United, Mbeya City, Ndanda FC, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na KMC ni miongoni mwa timu zilizo katika hatari hiyo.