Jumatatu , 6th Jan , 2020

Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) kupitia kwa Rais wake, Phares Magesa limesema kuwa Januari 14 hadi 18, 2020 timu ya taifa ya kikapu itashiriki mashindano ya kufuzu kucheza kombe la Afrika kwa wanaume, yatayofanyika Nairobi, Kenya.

Michuano ya Sprite Bball Kings 2019

Makocha walioteuliwa na kamati ya utendaji kuiongoza timu hiyo ni Alfred Ngalaji ambaye atasaidiana na Ashraf Haroun na makocha hao wameteua wachezaji watakaounda timu ya Taifa, ndani yake wakiwemo wachezaji wanne walioshiriki michuano ya Sprite Bball Kings 2019 ambayo huandaliwa na EATV na EA Radio kwa udhamini wa kinywaji cha Sprite, wakiwemo Baraka Sadick ambaye alishinda tuzo ya MVP.

Point Guards; Musa Chacha - JKT, Stephen Mshana - Vijana, Kaikai Lek - Savio

Shooting Guards; Sudi Ulanga - KIU, Uganda, Baraka Sadik - JKT, Erick John - Oilers, Ally Mohamed - JKT

Small Forwards; Enrico Augustino - ABC, Cornelius Peter - Savio, Ladislaus Lusajo - Eagles

Pewer Forwards; Amin Mkosa - Power, Uganda, Isaya Aswilie - Mbeya Flames, Fadhili Chuma - UCU, Uganda

Centers; Haji Mbegu - JKT, Mwalimu Heri - Vijana, Jackson Brown - JKT, Gwalugano John - Vijana, Jimmy Brown - Philippines

Vigezo vilivyotumika kuteua wachezaji hao ni uwezo wa mchezaji, uzoefu wa mashindano ya kimataifa na nidhamu ya mchezaji, timu hii ina wachezaji 17, kati yao 12 walikuwepo timu ya Taifa ya iliyoshiriki mashindano ya kanda ya tano, Kampala, Uganda mwaka jana na wachezaji 6 ni wapya ambao baadhi yao wameonekana kupitia Mtaka Taifa Cup 2019 iliyomaliza Simiyu mwezi Desemba 2019.

Wachezaji hawa wote wanatakiwa kuripoti kambini uwanja wa ndani wa Taifa tayari kwa kuanza mazoezi kuanzia kesho 7 Januari, 2020 na timu inatarajiwa kuondoka tarehe 12 Januari, 2020 kuelekea Nairobi, Kenya tayari kwa mashindano hayo.