Wanyama aiona nafasi ya Samatta EPL

Jumamosi , 6th Jul , 2019

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars', ambaye pia anakipiga katika klabu ya KRC GENK ya Ubelgiji Mbwana Samatta, amempongeza mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama haswa baada ya kukutana kwenye AFCON.

Mbwana Samatta (njano) na Victor Wanyama (nyekundu)

Samatta amefunguka kupitia mtandao wa Twitter ambapo amesema kuwa, alijivunia kukutana na kiungo huyo wa Tottenham kwenye mchezo wa Kundi C ambapo Kenya ilishinda kwa magoli 3-2.

"Ilikuwa ni nafasi nzuri kucheza na mmoja wa wachezaji bora na wa mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, tunajivunia uwepo wake ndani ya East Africa.", aliandika Samatta.

Kwa upande wake Wanyama amemjibu Samatta kwa kutoa shukrani zake. ''Nashukuru sana Kaka yangu, na ni matarajio yangu kukuona Premier League msimu ujao tuendelee kupeperusha bendera ya East Africa''.