
Waogeleaji
Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhani Namkoveka amesema, washiriki hao walichaguliwa kutoka katika Mashindano ya Taifa yaliyofanyika Machi na Novemba mwaka huu na wao kama chama wanaendelea kupokea majina ya uhakiki kwa wale waliochaguliwa na mpaka kesho watakuwa na orodha yote ya wachezaji na viongozi watakaoanza safari kwa makundi kuelekea Kigali kwa ajili ya mashindano hayo.
Namkoveka amesema, katika mashindano hayo wametoa nafasi mpaka kwa waogeleaji waliopo nje ya nchi ambao nao pia wanatakiwa kufanya uhakiki mapema ili kujua kama wataelekea moja kwa moja nchini Rwanda au watafika kwanza nchini Tanzania.
Namkoveka amesema, hapo awali waliambiwa watatumia bwawa la mita 25 katika mashindano hayo lakini leo wamepata taarifa kuwa watatumia bwawa la mita 50 taarifa ambazo bado wanasubiri uhakika ni bwawa gani litatumika huku kwa upande wao na washiriki kwa ujumla wakiwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo chini ya Kocha Felix Kalenga.