
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
Wenger alikutana na mmiliki wa klabu Stan Kroenke Jumatatu kutathmini mustakabali ujao wa Mfaransa huyo, na maamuzi zaidi yalirudishwa kwenye bodi ya wakurugenzi ya klabu.
Arsenal wanapanga kutoa taarifa maalum Jumatano, kumsimika tena Mfaransa huyo, aliyeweka rekodi mpya ya kushindwa kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21, tangu Arsenal imalize nafasi ya tano msimu uliomalizika.
Washika mitutu hao wa Emirates, walimaliza wakiwa pungufu ya pointi 18 nyuma ya mabingwa Chelsea, lakini waliifunga the Blues 2-1 kwenye fainali ya FA uwanja wa Wembley Jumamosi iliyopita.
Mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu, na ungehitimisha miaka 21 ya kocha huyo tangu ajiunge na timu hiyo, mwaka 1996.
Matukio ya kukumbukwa kwa Wenger;
Aliiongoza the Gunners kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza na makombe manne ya chama cha soka FA katika kipindi chake cha kwanza cha miaka 9.
Mnamo mwaka 2003-04, alikuja kuwa kocha wa kwanza tangu 1888-89 kuingia kwenye rekodi ya kutwaa ubingwa wa EPL bila ya kupoteza mechi.