
Yanga wanakutana na Mlale katika hatua hiyo ambapo mchezo huo ulitakiwa kuchezwa Machi mbili mwaka huu lakini kutokana na ratiba kubana wakaomba mchezo huo uchezwe wiki hii.
Yanga walituma maombi yao kwa shirikisho la soka nchini TFF wakitaka mchezo huo ufanyike wiki hii kutokana na kukabiliwa na mchezo wao wa kimataifa pamoja na kiporo cha Mtimbwa Sugar.
Yanga ilipiga hatua moja mbele katika michuano hiyo ya Kombe la FA baada ya kuitoa Friends Rangers kwa kuinyuka mabao 3-0 wakati JKT Mlale wakiitoa Majimaji hatua ya 32.
Mbali na mchezo huo, Yanga wanakabiliwa na mchezo mwingine siku ya Jumamosi hii dhidi ya Cercle de Joachim ukiwa ni mchezo wa kimataifa huku wakisubiri pia kiporo cha Mtibwa pamoja na mechi yao na Azam FC kunako ligi kuu ya soka Tanzania Bara.