Alhamisi , 4th Jun , 2020

Klabu ya Namungo FC imesema inapambana kuwabakiza wachezaji wao Bigilimana Blaize, Liliant Lusajo na Kocha Mkuu wa timu hiyo Hitimana Thierry, ambao wanahusishwa na kujiunga na klabu za Simba na Yanga.

Akiongea na EATV & Radio Digital, mwenyekiti wa Namungo FC, Hassan Zidadu amesema wako kwenye mchakato wa kuwabakiza wachezaji hao kutokana na mikataba yao kuelekea ukingoni.

Pia Zidadu amesema mipango ya Namungo FC kwa sasa ni kwenye kombe la FA ili wapate nafasi ya kuwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa, ambapo katika mechi ya Robo Fainali wamepangwa na Alliance FC.

Mtazame hapa akizungumza.