Alhamisi , 27th Jan , 2022

Kikosi cha timu ya wananchi Yanga SC kimefika jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa raundi ya 4 wa kombe la shirikisho Tanzania bara Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mbao FC.

Mashabiki wa Yanga SC jijini Mwanza wakimlaki kocha Nasreddine Nabi uwanja wa ndge baada ya timu kufika

Yanga itashuka dimba siku ya Jumamosi Januari 29 kuchza dhidi ya Mbao FC mchezo utakaochezwa katika dimba la CCM kirumba majira ya Saa 10:00 jioni. Awali mchezo huu ulipaswa kuchezwa jijini Dar es salaam kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa lakini siku hiyo uwanja huo utakuwa na matumizi mengine hivyo wenyeji wa mchezo huu klabu ya Yanga ikachagua uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wao wa nyumbani.

Timu ya wananchi wanaelekea kwenye mchezo huu wakiwa na rekodi nzuri dhidi ya Mbao kwani kwenye michezo 5 ya mwisho waliokutana na Yanga wameshinda michezo yote ukiwemo mchezo wa mwisho timu hizi kukutana Machi 20, 2020 mchezo ambao Yanga ilishinda kwa mabao 2-1.