
"Tshishimbi alikuwa amepewa muda kidogo wa kwa ajili ya kumalizia likizo yake na kumalizia michakato ya kujihakikishia kuja kufanya kazi nchini" . alisema Kaimu Msemaji wa Yanga Chicharito
Ikumbukwe Yanga tayari imecheza michezo miwili ya kujipima uwezo ambapo mchezo wa kwanza ikiwa mjini Morogoro ilicheza na timu ya vijana ya Moro Kids nakuididimiza timu hiyo kwa jumla ya mabao 5-0 na mchezo wa pili walikutana na timu ya matajiri wa alizeti Singida United na Yanga kuibuka na ushindi wa tabu wa mabao 3-2 katika mchezo uliochukua nafasi katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam.
Jumamosi wana Yanga watapata fursa ya kumuona kwa mara ya kwanza kiungo Mkongo, Papii Kabamba Tshishimbi akiichezea timu yao baada ya kusajiliwa kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland.
Aidha taarifa zinadai kuwa michezo yote miwili Yanga waliyonayo ni pamoja na Ruvu Shooting ambao unadhaniwa pia utachezwa huko Zanzibar.