Alhamisi , 4th Feb , 2021

Afisa Muhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz, ameweka wazi kuwa baada ya maelekezo ya FIFA tayari wameshaanza kushughulikia suala la kukamilisha malipo ya mchezaji wao wa zamani Amisi Tambwe ya takribani milioni 41.

Afisa Muhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz

Akiongea leo Februari 4, 2021 kwenye Kipenga Xtra ya East Africa Radio, Nugaz amesema ni kweli suala hilo walikuwa wanalijua lakini walichelewa kwasababu walikwenda CAS kwaajili ya kutafuta haki zaidi.

''Madeni yapo tu kwa kila taasisi ila hili limechelewa kwasababu lilikuwa kwenye mamlaka nyingine kama CAS, lakini sasa kwa maelekezo ya FIFA ndani ya siku tano tu malipo yatakamilika na hakuna shaka kwa mashabiki kuhusu timu yao kufungiwa'', amesema Nugaz.

Zaidi Tazama video hapo chini