Yanga yatwaa shambuliaji kutoka TP Mazembe

Jumatatu , 6th Jan , 2020

Mabingwa wa Kihistoria katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, hii leo imethibitisha kumpokea mshambuliaji kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Owe Bonganya.

Mshambuliaji Owe Bonganya (wa kwanza kushoto) akiwa na wakala wake pamoja na mwakilishi wa mdhamini wao.

Bonganya ametua pamoja na wakala wake anayejulikana kwa jina la Mutuale Nestoresangule, ambapo wamepokelewa na kiongozi wa juu wa GSM ambao ni wadhamini wao katika vifaa vya michezo.

Taarifa ya klabu ya Yanga imeeleza kuwa mchezaji huyo atajiunga moja kwa moja na timu iliyopo visiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.