Zakazakazi ataja sababu ya Azam kukosa ubingwa

Jumanne , 30th Jun , 2020

Mkuu wa Idara ya Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria 'Zakazakazi' amesema malengo ya klabu hiyo ni kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi licha ya kupitwa na wapinzani wao Yanga SC ambao anaamini wamekaa katika nafasi yake.

Afisa Habari wa Azam FC, Zakazakazi

Akifanya mahojiano maalumu na EATV & Radio Digital, Zakazakazi amesema mipango yao ya msimu huu ni kumaliza nafasi ya pili kwakuwa Simba SC tayari imeshabeba ubingwa huku akiweka wazi sababu iliyopelekea wao kukosa ubingwa kuwa ni kutokana na kubadilishwa kwa makocha.

Azam FC itajitupa dimbani kesho majira ya Saa 1:00 Usiku katika mtanange wa Robo Fainali ya Kombe la shirikisho dhidi ya Simba SC.