
Sergio Ramos akiwa kwenye moja ya mechi za Real Madrid
Si jambo rahisi kwa mchezaji kufikisha idadi hiyo ya magoli, bila kujali ni mchezaji wa nafasi gani uwanjani, hivyo kwa nafasi anayocheza Ramos ni jambo la kushangaza mno, wapo wachezaji waliocheza zaidi ya miaka 15 kwenye nafasi ya ushambuliaji lakini hawajafanikiwa kufikisha magoli 100,
Rekodi hiyo si ya kwanza kwa Ramos katika maisha yake ya soka, ana rekodi za aina zote mbili tofauti ambazo ni hasi na chanya, ikiwemo hii ya mlinzi wa kati kufunga magoli 100, kupiga na kufunga penati 23 mfululizo bila kukosa,lakini ndiye mchezaji mwenye kadi nyekundu nyingi kwenye la liga ambazo ni 20 na njano 191, kwenye UEFA ana kadi nyekundu 4 na njano 40,
Ramos alijiunga na Real Madrid mwaka 2005 akitokea Sevilla, tangu hapo amekuwa muhimili mkubwa ndani ya klabu hiyo na ameshiriki katika mafanikio yote ya klabu waliopata, ikiwemo na kutwaa ubingwa wa ligi mara 4 kombe la mfalme mara 2, kombe la supa cup 4 kombe la washindi Ulaya 4 na kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu mara 4,
Pia Ramos ndiyo nahodha wa timu ya Taifa ya Uhispania,na ni moja ya mchezaji mwenye mafanikio makubwa kwenye timu yake ya Taifa, ikiwemo kutwaa kombe la dunia la mwaka 2010 Africa kusini, kombe la Ulaya 2008 na 2012, ameandikisha rekodi kadhaa ikiwemo ya kuwa mchezaji mdogo kufikisha michezo 100 ya timu ya taifa mwaka 2013 na hadi sasa anajumla ya michezo 175,