Jumatano , 8th Jul , 2020

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden na klabu ya Ac Milan ametamba kuwa endapo angesajiliwa mapema katika klabu hiyo amaamini wangefanikiwa kutwaa ubingwa wa Scudetto msimu huu.

Mshambuliaji wa AC Milan,Zlatan Ibrahimovic(pichani),katika moja ya shambulizi kwenye mechi ya Seria A dhidi ya Juventus ambayo walishinda kwa bao 4-2.

Mshambuliaji wa klabu ya Ac Milan,Zlatan Ibrahimovic ametamba kwamba endapo angesajiliwa mapema kabla ya msimu kuanza,ana hakika wangetwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo msimu huu.

Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden ameyasema hayo baada ya kuisadia Ac Milan kuwanyuka mabingwa watetezi seria A,Juventus mabao 4-2,huku yeye akifunga moja kwa mkwaju wa penati na kutengeneza bao jingine la pili lililofungwa na Franck Kessie.

Mabao mengine ya Milan yalifungwa na Ante Rebic na Rafael Leao huku Juventus ilitangulia kuongoza kupitia Adrien Rabbiot na Cristiano Ronaldo.

Zlatan ambaye kwa sasa amefikisha umri wa miaka 38,amesema ni masikitiko kuwa alisajiliwa kati kati ya msimu,lakini kwa uwezo alionao licha ya nguvu zake kupungua kwa sasa,anaamini angechangia makubwa katika ubingwa msimu huu ambao hawajautwaa tangu mwaka 2011.

Katika hatua nyingine Zlatan ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Barcelona,Manchester United,Psg,,Inter Milan,Juventus kalba ya kurejea AC Milan ambayo aliichezea pia,amesema anatamani kuona mashabiki wanarejea viwanjani ili kunongesha michezo inayoendelea.

Tangu ajiunge na AC Milan,Zlatan amefunga mabao 6,katika mechi 13,Rossoneri imepoteza mechi mbili pekee na kupanda hadi nafasi ya 5 kwenye msimamo wa Seria A.

Hadi sasa Milan inayonolewa na kocha Stefano Pioli imefikisha alama 49 huku ikibakiwa na michezo saba kuumaliza msimu wa 2019/20.