Hayo ameyasema katika kikao na viongozi wa juu wa kamisheni hiyo kilichofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Aidha Allen amewahimiza viongozi hao juu ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa Kamisheni hiyo ambao haujafanyika kwa kipindi cha miaka miwili sasa.
Vilevile, Allen amewashauri viongozi wa TPBRC kuwa, wanapaswa kuongeza ushirikiano baina yao na BMT, na kuongeza juhudi katika uhamasishaji wa upatikanaji wa wanachama wengi zaidi kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa chama hicho.
