Jumatatu , 7th Sep , 2015

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuanza kukata umeme leo kwa mikoa inayotumia gridi ya taifa kwa wiki moja saa 12 kila siku ili kupisha uwashaji wa mitambo ya gesi kutoka Mtwara.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ugavi la umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba:

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba alitaja baadhi ya mikoa ambayo itakumbwa na tatizo hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Mbeya, Lindi, Mwara, Mwanza, Arusha na Mingine.

Mramba amesema wakati mitambo hiyo inayotumia gesi itakapozimwa, mtamboo pekee utakaobaki ukifanyakazi ni ubungo 1 ambao unaendesha mikoa michache ambayo haiko kwenye gridi ya taifa.

Amesema kama mradi huo utafanikiwa mitambo ya Symbion pekee itazalisha umeme wa megawati 102 mtambo wa ubungo 2 utazalisha megawati 105.