Ajali hiyo imetokea jana jioni katika hifadhi ya Taifa ya Selous wakiwa kwenye helkopta 5Y-DKK iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam kuelekea Ludewa Mkoani Njombe, ambapo kwa mujibu wa mtoto wa marehemu Slaa Jerry Slaa, helkopta hiyo ilipata matatizo ya injini.
Mpaka sasa bado haijajulikana kulikuwa na abiria wangapi kwenye helkopter hiyo ambao nao wamefariki dunia.
Tutaendelea kuwapa taarifa ya kitakachoendelea mara baada ya kupata kutoka kwenye timu ya uokoaji iliyopo eneo la tukio.