
Mshambuliaji wa Chelsea diego costa(kulia)akikabiliana na beki wa Arsenal Gabriel Paulista(kushoto)pichani
Bao pekee na la ushindi kwa The Blues lilifungwa na mshambuliaji wake matata Diego Costa dakika ya 23 ya mchezo kufuatia kros maridhawa ya Branislav Ivanovic.
Arsenal walicheza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya mlinzi wao Per Mertesacker, kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa.
Upungufu huo ulimfanya kocha Arsene Wenger, amtoe mshambuliaji Olivier Giroud, na kumwingiza mlinzi Gabriel Paulista.
Arsenal wameshindwa kufuta uteja kwa chelsea na kumewapelekea timu hiyo kushika nafasi ya tatu wakiwa na alama 44 huku Manchester City wakiwa katika nafasi ya pili kwa alama 44 na vinara ni Leicester City wakiwa na alama 47 kibindoni.