Jumanne , 3rd Mei , 2016

Meya wa Manispaa wa Ilala, ameagiza hatua za haraka za kinidhamu zichukuliwe kwa Daktari na Wauguzi wawili waliokuwa zamu siku ya Ijumaa katika hospitali ya Amana kwa kuchelewesha matibabu na kusababisha kifo cha mwendesha bodaboda.

Meya wa Manispaa wa Ilala, ameagiza hatua za haraka za kinidhamu zichukuliwe kwa Daktari na Wauguzi wawili waliokuwa zamu siku ya Ijumaa katika hospitali ya Amana kwa kuchelewesha matibabu na kusababisha kifo cha mwendesha bodaboda marehemu Solomoni Khamisi alijruhiwa mguuni baada ya kupigwa risasi na majambazi.

Meya huyo Charles Kuyeko amechukua hatua hiyo baada ya kusikiliza madaktari hao na ndugu wa mgonjwa na kubaini mgonjwa alishindwa kupata matibabu ya haraka kwa kushindwa kulipa kiasi cha elfu 20 kwa ajili ya kuongezewa damu jambo lililopelekea kuvuja damu na kupelekea kusababisha kifo chake

Katika utetezi wao madaktari walisema hakukuwa na damu ya kumuongezea mgonjwa huyo hospitalini hapo lakini Meya Kuyeko alipotembelea hifadhi ya damu ya hospitali hiyo akabaini kulikuwa na damu za kutosha ila mgomjwa huyo aliekuwa anavuja damu kwa kupigwa risasi hakuwa na fedha za kulipia huduma