Jumatano , 23rd Apr , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Kenya ambaye ameolewa huko Nigeria, Emmy Kosgei amekanusha uvumi ambao umeendelea kuenea kwa kasi kubwa kuwa yeye na mumewe wapo katika mpango wa kutengana baada ya ndoa yao kudumu kwa miezi 7 pekee.

Emmy ambaye kwa sasa yupo huko Boston kwaajili ya shughuli zake za kimuziki, amesema kuwa tetesi hizi zimeibukia mitandaoni, huku akiwaita wazushi wa taarifa zenyewe kuwa ni watu walioishiwa kazi za kufanya.

Emmy ambaye alifunga ndoa na pasta mwenye utajiri mkubwa kabisa huko Nigeria, Anselm Madubuko mwezi Agosti mwaka jana, katika uvumi huu, ametajwa kung'ang'ania talaka akiwa pia anadai mgawanyo wa mali za mumewe nusu kwa nusu.