
Tennis walemavu
Kocha wa mchezo huo Riziki Salum amesema, mashindano hayo ambayo yatakuwa ya mwisho kwa mwaka huu yatasaidia wachezaji wake kuwaandaa kwa mashindano ya Kenya pamoja na ya Afrika Kusini huku akiitaka Serikali na wadau wa mchezo huo kuisaidia timu hiyo na vifaa mbalimbali vya mchezo huo hususani viti ambavyo vitawasaidia katika mashindano hayo.
Kocha Riziki amesema, iwapo serikali na wadau watajitokeza kusaidia mchezo huo, katika mashindano ya mwakani wanaamini watafanya vizuri zaidi kwani hawatakuwa na changamoto nyingi kama ilivyo kwa mwaka huu ambapo wamejitahidi katika mashindano mbalimbali licha ya changamoto walizonazo.