Jumamosi , 5th Nov , 2016

Ndoa ya rapa mkali katika tasnia ya bongo fleva, Mabeste iliyofungwa hivi karibuni, hatimaye imezaa matunda baada ya mke wake aliyefunga naye ndoa hiyo kupata ujauzito.

Mabeste na Lissa ndani ya FNL

 

Mke wa mabeste ambaye ni mrembo na video qeen anayefahamika kwa jina la Lissa, amefunguka ukweli huo jana alipokuwa kwenye kipindi cha FNL, cha EATV  akiwa ameambatana na Mabeste, lakini akasita kutaja ujauzito huo kuwa ni wa miezi mingapi.

"Ni kweli, kwa sasa ni ujauzito, lakini kuhusu muda wa ujauzito huo siwezi kusema, hiyo ni siri ya familia" Alisema Lissa.

Kuhusu ni mtoto wa aina gani angependa kupata, Lissa amesema hachagui na kwamba yuko tayari kwa mtoto wa jinsi yoyote "Nataka iwe surprise"

Katika hatua nyingine Mabeste amekiri kuwa na furaha tangu akutane na mkewe huyo na hasa baada ya kufunga ndoa, huku akibainisha kuwa aliamua kufunga ndoa ya kimya kimya bila kuhusisha watu wengi kutokana na mazingira halisi aliyokuwa nayo.

Mabeste pia alifafanua jinsi alivyokutana na Lissa hadi kufikia hatua waliyofikia sasa huku akiweka wazi kuwa yeye ndiye aliyemshawishi Lissa wafunge ndoa.

Alisema alikutana na Lissa wakati akitafuta msichana wa kufanya naye video, na ndipo aliposhauriwa kumtumia Lissa licha ya kuwa ngumu kumshawishi

"Nilipukuwa natafuta 'video qeen', nikaambiwa kuna mtu anafaa, nilipomuona nikaona kweli atafaa, lakini nilipomueleza, alikataa sana, ingawa baadaye alikubali, kuanzia pale tukawa karibu zaidi hatimaye wapenzi hadi mke na mume" Alisema Mabeste

Kuhusu muziki Mabeste amesema anarejea kwa nguvu zote kwenye game kwa kuwa hata mkewe Lissa naye anamsapoti jambo ambalo Lissa mwenyewe anakiri na kusema kuwa asingependa Mabeste aache muziki