Jumatatu , 7th Nov , 2016

Vijana wametakiwa kutumia nguvu na taaluma walizonazo kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo na kuachana na utegemezi wa kusubiri ajira kutoka serikalini pekee.

Vijana wakijishughulisha na masuala ya ufundi.

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam, na Dkt. George Kahangwa, katika mkutano mkuu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Umoja wa watanzania (PANADET), na kusema kuwa maendeleo ya nchi hayawezi kuletwa na serikali pekee bila ya ushiriki wa wananchi.

Dkt. Kahangwa amesema kuwa kila sekta nchi ina nafasi kwa upande wake katika kuchangia maendeleo hivyo vijana hawana budi kutafuta fursa mbalimbali katika ushiriki wao wa kukuza uchumi wa nchini.

Kwa upande wake mwanzilishi wa taasisi hiyo bi. Elizabeth Mhagama, amesema kwa ushirikiano katika kuleta maendeleo ya kiuchumi utasaidia kuunga mkono jitihada za serikali za kuwafanya watanzania kuwa na vipato vya kati.