Boniventura Mwalongo - Katibu Mkuu TRAMEPRO
Watu hao huwarubuni watoa tiba asili nchini kiasi kikubwa cha pesa huku wakitumia majina ya viongozi wakubwa wa kitaifa katika utapeli wao huo.
Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asili na Ulinzi wa Mazingira nchini Tanzania – TRAMEPRO, Bw. Boniventura Mwalongo, ametoa wito huo alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya uwepo wa kundi hilo la matapeli ambalo linadaiwa kutekeleza uhalifu huo katika mikoa kadhaa nchini.
Mwalongo ameishauri Wizara ya Mambo ya Ndani kusimamia sheria kwa kuhakikisha kuwa hakuna mtoa tiba asili anayefanya shughuli za tiba na usajili wa watoa tiba pasipo kutambulika na serikali hususani wizara hiyo.

