AT
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, AT amesema alishawaambia siku nyingi kuwa msanii mzuri ni yule ambaye anafanya muziki wa tofauti na bado akawa kwenye hit, huku akitolea mfano muziki wa Ojuelegba wa Wizkid na muziki wa Darasa wa sasa,
AT amesema iwapo msanii atafanya kitu cha tofauti na kuonyesha ulimwengu utofauti wake na bado watu wakamuelewa, haina sababu ya kutokubali kumsifia.
"Kuna watu wana desturi ya kutokuelewa vitu, nilizungumza na nikasema msanii mzuri sio yule mwenye lundo la macollaboration, msanii mzuri ni yule ambaye atafanya aina tofauti ya muziki na wenziwe, mi ningependa niwaambie mwenzio akifanya vizuri actualy msifie kafanya tofauti kafanya, na hii imejitokeza mfano ni wimbo wa Ojuelegba, mfano Aje, mfano mwengine ni ngoma ya Darasa, aina tofauti na muziki wanaofanya wenzio ukifanya utakuwa ni msanii mzuri", alisema AT.
AT aliendelea kusema kuwa .......... "kwa hiyo akili zangu muwe mnajaribu kuzifanyia kazi na kuziweka katika vitabu vya kumbukumbu, hizi akili sio 0 Kb, hii terabite MG au Gigabite hizi akili",alisema AT.