Jumamosi , 5th Oct , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuna maswali huwa anajiuliza, lakini majibu yake yanampa nguvu ya kuendelea kuwatumikia Watanzania.

Rais Magufuli

Rais Magufuli ameyasema hayo jana Oktoba 4, 2019, wakati akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Songwe, kwenye mkutano wa hadhara katika ziara yake mkoani humo , ambapo alisema kila akifikiria kuondoka kuna maswali mengi anajiuliza na anapata jibu la kuendelea.

''Kuna muda ukikaa unajiuliza mateso waliyokuwa wanapata watu unaona ilikuwa lazima tu nifanye kazi, nikitazama leo nikiiacha nchi, Ndege zitanunuliwa? SGR itajengwa? Vituo vya afya vitajengwa? Stiegler's Gorge itajengwa? Je miradi yote itatekelezwa?, hapo ndipo ninajisikia lazima niendelee'', amesema.

Aidha Rais Maguguli amewaomba watanzania kuendelea kumuombea yeye pamoja na Mawaziri, kwani wanafanyakazi kwa mateso makubwa sana.

''Katika kipindi ambacho Mawaziri hawakufaidika ni wakati wangu, hata anapolala hajui kama kesho ataamka akiwa waziri', ameeleza.

Zaidi tazama Video hapa chini.