Msanii wa vichekesho Idris Sultan na mwenzake Innocent Maiga, wakiwa katika Mahakamani.
Idris amepandishwa kizimbani na mwenzake Innocent Maiga, ambaye ameshtakiwa kwa kosa la kutokuripoti mabadiliko ya umiliki wa laini hiyo, ambayo inatumiwa na Idris .
Katika mashtaka hayo wote kwa pamoja wameyakana na kuachiwa kwa dhamana ya kiasi cha shilingi Milioni 15, ambapo keshi hiyo itatajwa tena Juni 9, 2020.
Watuhumiwa wote wawili, wanadaiwa kuyatenda makosa hayo kati ya Disemba 1, 2019 na Mei 19, 2020, maeneo ya Mbezi Beach katika Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.