Jumatano , 8th Jul , 2020

Kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amesema atazungumza na beki John Stones mwishoni mwa msimu huu ili kujua hatma yake iwapo atasalia kwenye kikosi chake au ataondoka.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola akimpa maelekezo beki Jone Stones katika moja ya mechi ya ligi kuu ya England

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amesema atafanya mazungumzo na beki John Stones mwishoni mwa msimu huu ili kujua hatma ya mchezaji huyo kama atasalia au ataondoka kattika kikosi chake.

Stones raia wa England amekua akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara toka ajiunge na City akitokea Everton mwaka 2016, hali inayosababisha akose nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Kukosekana kwa utimamu wa mwili wa Stones kunasababisha ashindwe kupigania namba katika idara ya ulinzi ambayo inawachezaji wengi wenye ubora akiwemo Aymeric Laporte,Eric Garcia,Nicolas Otamend na hata Fernandinho.

Imeripotiwa kuwa mkataba wa beki huyo unamalizika mwaka 2022 na tayari vilabu vya Arsenal na waajiri wake wa zamani Everton wameonyesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Msimu huu Stones amejikuta akicheza michezo 12 tu ya ligi kuu na 20 katika michuano yote kutokana na kusumbuliwa  na majeruhi ya kifundo cha mguu.