Alhamisi , 29th Oct , 2020

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Marcus Rashford alifunga hat trick akitokea benchi wakati mashetani wekundu wakiichapa RB Leipzig kwa bao 5-0 katika mchezo wa kundi H.

Marcus Rashford akipachika moja ya bao kati ya matatu aliyoyafunga dhidi ya RB Leipzig .

Rashford aliingia dakika ya 64 akichukua nafasi ya Mason Greenwood ambaye alifunga bao na kupachika mabao dakika za 74, 78, na 90.

Mabao hayo matatu yanamfanya Rashford kuwa kinara wa ufungaji akiwa amefikisha mabao manne katika mechi mbili alizocheza.

Mabao mengine ya Manchester United yalifungwa na Mason Greenwood na Antony Martial aliyepachika kwa mkwaju wa penati dakika ya 87.

Huo ni ushindi wa pili kwa Manchester United katika kundi hilo baada ya wiki iliyopita kuichakaza PSG kwa bao 2-1 ugenini.

Kimekua kiwango bora kwa mashetani wekundu ambapo tangu wafungwe bao 6-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs, wameshinda mechi tatu mfululizo katika mashindano yote, sare moja .

Matokeo mengine ya kundi hilo, Psg iliibuka na ushindi wa bao 2-0 zote zikifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Juventus na Everton, Moise Keane ambapo matajiri hao waliwanyuka Instanbul Basaksehir ya Uturuki.

Katika mchezo huo, habari mbaya ni juu ya kuumia kwa Neymar Jr.

MATOKEO MENGINE

FC Krasnodar 0-4 Chelsea

Sevilla 1-0 Rennes

Barcelona 2-0 Juventus

Ferencvaros 2-Dynamo Kyiv

Borussia Dortmund 2-0 Zenit st Petersburg

Clubb Brugge1-1 Lazio