
Zitto Kabwe
Zitto ameripoti Polisi ikiwa ni kutekeleza agizo alilopewa na Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, alipokamatwa na kuachiwa Novemba 3, 2020.
Baada ya kuripoti kituoni hapo leo, Zitto ameambiwa afanye hivyo tena siku ya Ijumaa Novemba 13, 2020. ''Kila baada ya siku 2 tunaripoti Kituo cha Polisi Oysterbay. Nimetoka kuripoti leo na nimeambiwa nirudi tena Ijumaa'', amesema Zitto.
Aidha ameongeza kuwa, ''Hii itaendelea mpaka hapo watawala watakapoamua ama kutupeleka Mahakamani au kutupilia mbali tuhuma wanazotushtaki nazo''.