Jumatatu , 16th Nov , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaambia wananchi  na viongozi kuwa kazi ya uwaziri mkuu haina dhamana huku akisema  ili waziri mkuu Kassim Majaliwa abaki kwenye nafasi hiyo kwa muhula wote  itategemea na utendaji wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Akizungumza leo Ikulu Chamwino mara baada ya kuwaapisha mawaziri wapya,Magufuli amesema kuwa wakati anampendekeza Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania hakutaja kwamba atakaa kwa muda miaka mitano kama ambavyo watu wengi wanasema.

“Nataka niwaambie waheshimiwa wabunge na nataka nimwambie Waziri Kassim Majaliwa na watanzani kazi ya uwaziri mkuu haina dhamna nilitaka nizungumze hili na yeye aelewe itategemea na utendaji kazi  yake, tumuombee afikie kwenye rekodi  ya Sumaye miaka aliyonayo ni mitano hiyo mingine ni  ‘probability’ ” amesema Rais Magufuli

Aidha Rais Magufuli ameongeza pia, “Kazi hii ya uongozi ni ngumu sana, nafahamu changamoto anazozipata waziri Majaliwa, Majaliwa ni mchapakazi na muadilifu sana, ukimtuma kitu anakwenda anakitekeleza na anakibeba kama chake anafahamu uongozi na lengo analifahamu na ndio maana sikupata shida kumteua”