Alhamisi , 3rd Dec , 2020

Dj wa zamani wa msanii Nay Wa Mitego Dj Msabato amefunguka kusema chanzo cha kuacha kufanya kazi na msanii huyo ni kufumania ujumbe 'message' kwenye simu ya mwanamke wake akiwa anamtaka kuwa naye kwenye mahusiano.

Kushoto ni Dj Msabato, kulia ni Nay wa Mitego

Dj Msabato amesema jambo hilo lilipelekea kukwazana na 'boss' wake ambapo kulitokea tofauti kati yao hadi alipoamua kuacha kufanya kazi pamoja.

"Kuna mwanamke wangu alitaka kumuiba nikawa sijapenda hilo suala baada ya kumfuata akawa anabisha wakati kuna message zilikuwa zinaonekana kwamba ni kweli alikuwa anamtongoza mwanamke wangu ambaye nilimchagua, nilijaribu kumwambia lakini alikuwa anakataa nikaamua kutoka ili tusifikie pabaya" amesema Dj Msabato

Tumejaribu kumtafuta Nay wa Mitego kwa njia ya simu lakini bahati mbaya hakuweza kushika simu yake ili kujibu madai ya tuhuma hizo.