Jumanne , 9th Mar , 2021

Cristiano Ronaldo anarejea kwenye kikosi cha Juventus kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora leo usiku Machi 9, 2021, dhidi ya FC Porto ya Ureno.

Cristiano Ronaldo

Katika mchezo huo Juventus wana kibarua cha kupindua matokea baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 alianzia benchi kwenye mchezo wa ligi 'Serie A’ Jumamosi iliyopita dhidi ya Lazio, mchezo ambao walishinda bao 3-1, Ronaldo aliingia dakika ya 69 akichukua nafasi ya Alvaro Morata.

Kuelekea mchezo huo Kocha wa Juventus Andrea Pirlo amesema, “Cristiano yupo vizuri, hizi ndio mechi zake ni wamoto, amepumzika na anasubiri kwa hamu. Tunajua kuna shinikizo kubwa kwetu, tuna kila sababu yakusonga mbele, sisi ni Juventus tunapaswa kufikiria juu ya kufuzu”.

Msimu uliopita kibibi kizee cha Turin Juventus walitolewa kwenye hatua kama hii na Olympic Lyon ya Ufaransa, na katika mchezo wa usiku wa leo dhidi ya FC Porto wanahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali.

Mchezo mwingine wa ligi ya mabingwa Ulaya utakaopigwa leo usiku, Borussia Dortmund ya Ujerumani watakuwa wenyeji wa Sevilla ya Hispanaia, mchezo wa mkondo wa kwanza Dortmund walishinda kwa mabao 3-2.