
Mhe. Kwandikwa amesema hayo akijibu swali liloulizwa na Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya liliosema, “Je, katika kuhakikisha mnajipanga vizuri kwanini msihakikishe mafunzo ya silaha wanapewa watu kadhaa ambao mnajua wataajiriwa kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na wengine ambao hawaajiriwi wapewe mafunzo ya ujasiriamali ili wajiajiri wenyewe kwani sio wote wanapokea mafunzo hayo ni wakuaminika”.
Akijibu swali hilo Mh. Kwandikwa amesema “Upo utaratibu mzuri wa kufanya mafunzo hatufanyi mafunzo kiholela tunafanya kulingana na mahitaji na matumizi ya nguvu ya kazi ya vijana tuliokuwa nao, nimhakikishie Mhe. mbunge mafunzo haya tunayofanya yanadhamira ya kulifanya taifa letu likae katika hali nzuri”.
Awali akielezea sababu ya kurudishwa nyumbani vijana ambao walishafika kambini kwa mafunzo ya JKT Kwandika amesema ni kwa jili ya JKT kujitathimi mafunzo yaliyofanyika na kuandaa utaratibu wa kuwa na mitaala bora itakayowawezesha vijana kujitegemea mara wanapomaliza mafunzo sambamba na kuongeza muda wa mafunzo kwa mujibu wa sheria kuwa mwaka mmoja badala ya miezi mitatu.
“JKT ilisitisha mafunzo ya vijana wa kujityolea kwa mwaka wa fedha 2020/21 kutokana na sababu zifuatazo; kutoa nafasi kwa JKT kutathimini mafunzo yaliyofanyika na Kuandaa utaratibu wakuwa na mitaala bora ya mafunzo ya vijana itakayowezesha vijana kujitegemea mara wakimaliza mafunzo badala ya kutegemea kuajiriwa” amesema Waziri Kwandikwa.