
Kocha mkuu wa mabingwa wa NBA msimu wa mwaka 2020-2021 timu ya Milwaukee Bucks, Mike Budenholzer akishikilia tuzo ya kocha bora wa msimu wa mwaka 2018-2019 aliyeipata msimu wa kwanza alipotua Bucks.
Baada ya Budenholzer kaongeza kandarasi hiyo ambayo thamani yake haijawekwa wazi, Wamiliki wa timu hiyo Marc Lasry, Wes Edens na Jamie Dinan wote kwa pamoja wamemwagia sifa kocha huyo kwa kusema ni kocha bora na mwenye uzoefu mkubwa hivyo wanajivunia sana.
“Ilikuwa ni safari yakusisimua hadi kufikia hatua ya kushinda ubingwa wa NBA msimu uliopita kitu ambacho kinatufanya tuthamini ubora wake na kuona ni jinsi gani ni vigumu kushinda taji hilo na ni fahari kuwa na kocha bora na wachezaji bora kuwa kwenye nafasi ya kufanya hivyo”. Alisema Marc Lasry.
“Mike ana uongozi imara sana, jopo la makocha lenye taaluma, wamethamiria kufanya maendeleo ya kukuza wachezaji na kuwa na muunganiko wa kufanyakazi kwa pamoja kushindana na kubeba makombe”. Amesema Wes Edens.
Budenholzer ameongeza mkataba huo baada ya kuwasaidia wakali hao kubeba ubingwa wa kwanza wa NBA tokea msimu wa mwaka 1971 na kuzidi kuimaraisha kikosi hicho kuwa na ushindani zaidi kwa kuwaunganisha nyota wakali wakiwemo, Giannis Antentokounmpo na Khris Middleton.
Mbali na nyota hao, Bucks ina wakali kama vile Jrue Holiday na Brook Lopez ambao wote kwa pamoja walishiriki kubeba ubingwa huo, huku Giannis, Middleton na Holiday walishuhudiwa wakichuana na nyota wengine kuwania tuzo ya mchezaji bora wa fainali za NBA na hatimaye tuzo hiyo ikaenda kwa Giannis Atentokounmpo.
Budenholzer alijiunga na Bucks msimu wa mwaka 2018 na kuisaidia timu hiyo kurudisha kamali yake hadi kumpelekea kuwa kocha bora wa msimu wa mwaka 2018-2019 pamoja na rekodi pekee ya kibabe ya kushinda michezo 165 na kufungwa 25 ikiwa ndiyo timu pekee iliyoongoza kwa kufunga zaidi ndani ya misimu mitatu ambayo Budenholzer alipotua Bukcs.