Ijumaa , 27th Aug , 2021

Msanii Pasha Mtepa anasema watu wanamkosea heshima kumshindanisha na Harmonize kwa sababu yeye ndio wa kwanza kuuwakilisha mkoa wa Mtwara na amekaa muda mrefu kwenye game.

Picha ya Pasha kulia, kushoto ni Harmonize

Akizungumza na eNewz ya East Africa TV Pasha anasema wasanii wote wanaowakilisha mkoa wa Mtwara wanafanya vizuri kuanzia Harmonize, Ibraah na Kinata MC ila hataki kushindanishwa na Harmonize.

"Unanikosea heshima kunishindanisha na Harmonize, mimi nimefanya vikubwa sana nimekaa miaka 7 bila ngoma kabla yeye hajatokea lakini nimeishika mioyo ya wana Mtwara, nimewaheshimisha na wanajivunia kuhusu mimi," amesema Pasha.

Pasha amemaliza kusema kila mtu aachwe katika nafasi yake kwa sababu kila mtu anafanya vizuri kwa upande wake.