Jumamosi , 22nd Jan , 2022

Kufuatia hali ya ukame na ukosefu wa malisho unaoukabili mkoa wa Kilimanjaro umepelekea jumla ya ng'ombe 841, kondoo 406 na punda 10 kufa.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 22, 2022, na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai, wakati akizungumza mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni linalofanyika mkoani humo.

"Changamoto kubwa inayotukabili ni kutonyesha kwa mvua za vuli hali iliyosababisha ukame na ukosefu wa malisho katika wilaya za Same na Mwanga, ambapo jumla ya Ng'ombe 841, Kondoo 406 na Punda 10, wameripotiwa kufa kwa kukosa malisho na maji," amesema RC Kagaigai