
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya Muungano wa Afrika AU Moussa Faki, ambaye pia ni Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad , amesema kupitia ukurasa wake wa twita kuwa amepokea maombi mapya ya Rais Zelensky , wakati alipowasiliana kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine .
Pia kulikua na majadiliano ya mengine yaliyohusu matakwa ya Ukraine kuendeleza ushirikiano wea karibu na Umoja wa Afrika.
Hata hivyo Bw. Faki hakuweka wazi endapo kama ombi hilo litakubaliwa , lakini kupitia ukurasa huo wa twita amesisitiza kwamba amani ndio suluhu pekee inayohitajika kwenye vita hivyo vya Russia.
Mapema mwezi huu , Rais Zelensky aliwasiliana kwa njia ya simu na Rais wa Senegal Macky Sall, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa umoja wa Afrika (AU) akimuomba kuwahutubia viongozi wa bara la Afrika.
Nchi za Africa zimeungana kwa wingi na nchi zingine ambazo hazikupiga kura kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa juu ya kuiondoa Russia kutoka kwenye baraza la haki la UN .
Matokeo yanaonesha kuwa azimio hilo lilipigiwa kura za ndio zipatazo 93 , sio zipatazo 24 , na ambao ambao hawakupiga kura ni mtaifa 58